MATOKEO YA MGOMO SHULENI
Athari za mgomo wa walimu wa shule za upili ambao umeingia siku ya 8 sasa zimeanza kuonekana wazi wazi, baada ya baadhi ya shule kuwataka wanafunzi waondoke na kurejea nyumbani hadi suluhu litakapopatikana.
Baadhi ya shule hizo ni ile ya wasichana na wavulana ya Kenyatta katika kaunti ya Nakuru, ambapo wazazi wamefika shuleni humo mapema leo baada ya kuagizwa wafike kuwachukua wanao.
Haya yanajiri wakati ambapo walumu wameapa kuendelea kulemaza masomo katika shule za upili za umma.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































