THE BLUES YAWINDA JHON DURAN

Klabu ya Chelsea inawinda huduma za mchezaji wa Aston Villa na raia wa Colombia Jhon Duran,21 ili kuimarisha safu ya ushambulizi.
Duran amefunga mabao matano ya ligi,nane kwa jumla ukiongeza mechi za ligi ya Europa licha ya kuwa mbadala wa Ollie Watkins.
Chelsea wapo kwenye mazungumzo ya juu ya kutaka kumsajili mshambuliaji wa Aston Villa na Colombia Jhon Duran, kulingana na ripoti kutoka majarida ya spoti.
The Blues wamekuwa wakisaka mshambuliaji, baada ya kuhusishwa kwanza na Victor Osimhen, kisha Benjamin Sesko, ambaye ameamua kusalia Ujerumani, kabla ya kurejea tena kutaka kumnunua Duran kutoka Villa.
Gazeti la En La Jugada linaripoti kuwa,Chelsea wana makubaliano na Villa kwa ajili ya Duran kwa zaidi ya mara mbili ya bei waliyolipa kutoka MLS, na mkataba huo unakaribia kufikia pauni milioni 40.
Msimu uliopita ,Chelsea walimtaka mshambuliaji huyo wa Colombia lakini wakaachana na nia yao na kuelekeza nguvu zao kwa Sesko ambaye kwa sasa amesaini mkataba mwingine na RB Leipzig.Uamuzi wa mchezaji huyo,umeifanya Chelsea kuharakisha mazungumzo na Villa ili kumpata Duran.
Licha ya kuwa mbadala wa Ollie Watkins, Duran alifunga mabao matano ya ligi, nane kwa jumla ukiongeza mechi za ligi ya Europa.
Mwezi uliopita, ajenti wa Duran, Jonathan Herrera alidokeza kwamba mchezaji huyo anaweza kuondoka baada ya kukiri kuwa mchezaji huyo hapati muda mwingi wa kucheza. Aliiambia El VBar Caracol ya Colombia:
imetayarishwa na Nelson Andati