#Local News

KOOME AAGIZA MAHAKAMA KUENDELEZA HUDUMA

Jaji mkuu Martha Koome ameziamuru mahakama zote nchini kuendelea kutoa huduma isipokuwa ile ya Makadara, na kusitisha matumizi ya mahakama za muda, akiwataka majaji na mahakimu kutumia mahakama za mtandao.

Katika taarifa kwa vyombo vya habari, Koome amesema hatua hiyo inalenga kuimarisha usalama wa maafisa wa idara ya mahakama.

Aidha, Koome amesikitika kwamba katika siku za awali, idara yake imekuwa ikiirai bunge na serikali tendaji kuongeza mgao wa kuiwezesha kuimarisha utoaji wa huduma za mahakama bila mafanikio.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *