MBAPPE APATA NAFUU
Kocha wa Ufaransa Didier Deschamps amefichua kwamba Kylian Mbappe anaimarika kila siku” lakini hakuthibitisha kama nahodha wake angeanza mechi ya mwisho ya kundi la Euro 2024 leo dhidi ya Poland.
Mbappe hakushiriki katika sare ya 0-0 na Uholanzi Ijumaa iliyopita mjini Leipzig baada ya kuvunjika pua kwenye ushindi wa 1-0 wa timu yake dhidi ya Austria mjini Duesseldorf wiki moja iliyopita.
Deschamps aliongeza kua kwamba barakoa inamzuia kwa kiasi fulani lakini inazuia uwezo wake wa kuona kidogo.
Ufaransa wanaingia kwenye mchezo wakiwa nafasi ya pili kwenye kundi na nafasi yao katika hatua ya 16 bora ikiwa na shaka kidogo.
Hata hivyo, washindi wa pili wa Kombe la Dunia 2022 wanahitaji kuboresha matokeo ya Uholanzi kwa wakati mmoja dhidi ya Austria — au angalau kushinda kwa tofauti kubwa — ili kuchukua nafasi ya kwanza.
Wana nia ya kumrejesha nyota wao mbele uwanjani kutokana na bao lao pekee hadi sasa katika mechi mbili lilikuwa la kujifunga.
Imetayarishwa na Nelson Andati
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































