NAIROBI UNITED WANA IMANI YA KUPANDA DARAJA

Kocha wa Nairobi United Edwin Mwaura anaamini bado wako mbioni kupandisha daraja la Ligi Kuu ya NSL/FKF na kufuzu kwa mchujo.
Naivas wanashikilia nafasi ya tatu kwenye msimamo wakiwa na alama 67 huku Nairobi United wakiwa nafasi ya nne wakiwa na alama 63. Tayari, Mara Sugar na Mathare United zimefunga nafasi mbili za kufuzu.
Klabu hiyo itawakaribisha Migori Youth siku ya Jumamosi katika viwanja vya Mpesa Foundation Academy katika awamu ya mchujo ya michezo ya NSL. Naivas watakuwa wenyeji wa Gusii FC walioshuka daraja katika uwanja wa Kenyatta mjini Machako.
Imetayarishwa na Janice Marete