ANDUGU ANA MATUMAINI YA MSIMU UJAO

Katibu Mkuu wa AFC Leopards Gilbert Andugu anatumai kuwa timu hiyo itashinda mechi zao zote zilizosalia ili kumaliza msimu wa ligi kuu ya msimu wa mwaka wa 2023/24 kwa kasi.
Ingwe kwa sasa wako nafasi ya sita kwenye jedwali wakiwa na alama 47, moja nyuma ya Bandari iliyo nafasi ya nne kuelekea Shabana tarehe 15 mwezi huu.
Andugu pia amewahamasisha mashabiki wa Ingwe kujitokeza kwa wingi dhidi ya Shabana ili kuishangilia timu yao wakati ligi hiyo ikikaribia kumalizika.
Imetayarishwa na Nelson Andati.