#Sports #Tennis

KOCHA MURRAY ATOA WITO KWA SERIKALI

Kocha mashuhuri wa tenisi Judith Murray ambaye ni mamake nyota mstaafu wa mchezo huo kutoka Uingereza Andy Murray, ametoa wito wa kuweko kwa mpango mahususi wa ukuzaji wa vipaji ikiwa Kenya inataka kufanikiwa katika mchezo huo.

Kulingana na Murray, mafanikio katika tenisi hayapatikani tu kwa kuwa na vifaa vizuri peke yake, akisisitiza juu ya umuhimu wa kupata makocha wenye uzoefu, washirika wazuri mazoezini, na programu maalum za mazoezi ya tenisi.

Alibainisha kuwa ufadhili mzuri na mpango mbadala ni muhimu kwa wachezaji wanaolenga kufika kileleni bila kujali mtu anatoka wapi.

Judith Murray aliyasema hayo alipokuwa katika uwanaj wa Sadili Oval mtaani Langata, hapa Nairobi ambapo aliongoza kliniki ya mafunzo kwa wachezaji wanaoenukia.

Imetayarishwa na Nelson Andati

KOCHA MURRAY ATOA WITO KWA SERIKALI

BADO HATUJAANZA MAZOEZI MUHAMBE ASEMA

KOCHA MURRAY ATOA WITO KWA SERIKALI

KABRAS WALAMBA SUKARI

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *