#Football #Sports

ANGEL DI MARIA AISAIDIA ARGENTINA KUTUA USHINDI

Bao La Angel Di Maria Liliiwezesha Argentina Kushinda 1-0 Dhidi Ya Ecuador Katika Mechi Ya Kirafiki Ya Kabla Ya Copa America Mjini Chicago Jumapili.

Di Maria, Ambaye Atastaafu Kucheza Soka La Kimataifa Baada Ya Copa America, Aliifungia Argentina Dakika Tano Kabla Ya Kipindi Cha Mapumziko Baada Ya Kuuwahi Mpira Wa Cristian Romero.

Argentina Itamenyana Na Guatemala Katika Mechi Nyingine Ya Kirafiki Siku Ya Ijumaa Kabla Ya Mabingwa Hao Watetezi Kuanza Kampeni Ya Copa America Dhidi Ya Canada Juni 20. Kisha Watacheza Na Chile Siku Tano Baadaye Na Peru Juni 29.

Ecuador Watamenyana Na Bolivia Siku Ya Jumatano Na Honduras Jumapili Kama Sehemu Ya Maandalizi Yao Ya Copa America. Wanaanza Kampeni Zao Katika Mchuano Wa Robo Mwaka Dhidi Ya Venezuela Mnamo Juni 22 Kabla Ya Kumenyana Na Jamaica Siku Nne Baadaye Na Mexico Juni 30.

Michuano Ya Copa America Itafanyika Nchini Marekani Kuanzia Juni 20 Hadi Julai 14.

Imetayarishwa na Nelson Andati

ANGEL DI MARIA AISAIDIA ARGENTINA KUTUA USHINDI

STRATHMORE BLADES WAONYESHA MAKALI YAO

ANGEL DI MARIA AISAIDIA ARGENTINA KUTUA USHINDI

FRANCE WATOKA SARE NA CANADA.

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *