OKWEMBA ATAKA UWEKEZAJI KWA CHIPUKIZI KUINUA SOKA

Kiungo wa zamani wa AFC Leopards, Charles Okwemba, anawataka wadau wa soka nchini kuwekeza kwa wachezaji chipukizi ili kuwawezesha kuwa na ushindani kwenye ngazi ya kimataifa.
Wito wake unajiri siku chache baada ya timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 20, Rising Stars, kuondolewa kwenye mashindano ya AFCON U20 nchini Misri bila kushinda mechi yoyote, baada ya kupoteza dhidi ya Morocco na Tunisia na kutoka sare ya 2-2 na Nigeria, na hivyo kumaliza mkiani katika kundi lao.
Okwemba, ambaye pia aliwahi kuchezea Vihiga United FC mwanzoni mwa taaluma yake, anasisitiza kuwa soka ya mashinani inapaswa kupewa kipaumbele ili kuibua vipaji kutoka utotoni. Aidha, anawataka viongozi wa soka kubuni mikakati mipya ili kuhuisha tena kiwango cha mchezo huo nchini.
Imetayarishwa na Janice Marete