WAWEKEZAJI WA SUKARI KUKABILIWA NA UHAKIKI WA MIKATABA
Mikataba ya wawekezaji binafsi waliokabidhiwa kusimamia viwanda vya sukari huenda ikafutiliwa mbali endapo hawatatekeleza wajibu wao ipasavyo.
Afisa Mkuu Mtendaji wa Bodi ya Sukari, Judy Chesire, amesema kuwa wawekezaji hao wanapaswa kuhakikisha wanalipa wakulima wa miwa kila wiki, kuendeleza kilimo cha miwa, pamoja na kutumia mitambo ya kisasa katika usagaji wa miwa.
Ameongeza kuwa mikataba yao ya muda wa miaka 30 ilizingatia kiwango kikubwa cha uwekezaji kinachohitajika katika sekta hiyo.
Imetayarishwa na Janice Marete
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































