#Local News

MWANAHARAKATI NJAGI, NDUGU WAWILI WAPATIKANA HAI

Ni afueni kwa familia za mwanaharakati Bob Njagi na ndugu wawili Aslam na Jamil Longton waliokuwa wametoweka kwa mwezi mmoja kupatikana wakiwa hai.

Taarifa za kupatikana kwa watatu hao zimewekwa wazi na Rais wa chama cha wanasheria nchini LSK Faith Odhiambo, ambaye amesema kuwa Njagi amejiwasilisha usiku wa manane katika kituo cha polisi cha Tigoni baada ya kutupwa maeneo yaliyo karibu na kituo hicho.

Aidha, amesema ndugu wawili Longton, wamepatikana hai wakiwa wametupwa katika eneo la Gachie, saa chache baada ya inspekta mkuu wa polisi Douglas Kanja na mkurugenzi waw a idara ya jinai DCI Mohammed Amin kukana kwamba polisi hawakuhusika kwenye utekaji nyara wa watatu hao.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

MWANAHARAKATI NJAGI, NDUGU WAWILI WAPATIKANA HAI

SHULE YA MUMBUNI MACHAKOS YAFUNGWA

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *