#Local News

MAAMBUKIZI YA VIRUSI VYA HIV YAPUNGUA KENYA

Wizara ya afya imetangaza kupungua kwa maambukizi ya virusi vya HIV kwa asilimia 68.

Kwa mujibu wa wizara ya afya mambukizi ya HIV kutoka kwa wamama wajawazito hadi kwa Watoto wao vile vile yamepungua kwa asilimia 65.

Akizungumza katika kongamano la kuimarisha utoaji wa huduma za HIV mkuu wa idara ya afya ya familia katika wizara ya afya Bashir Isaac amekiri kwamba idara ya waadhiriwa ambao wanapokea matibabu imefikia milioni nne.

Bashir  amesema pia idadi ya wakenya wanaojitokeza kujua hali yao ya HIV imeongezeka kwa kati asilimia 74-78.

Imetayarishwa na Janice Marete

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *