JUHUDI ZA SERIKALI KUKABILI MPOX

Wizara ya afya imetangaza kwamba taifa linajizatiti kuweka mikakati ya kuzuia mlipiko wa ugonjwa wa Mpox na wala si kutibu, na kuhimiza ushirikiano wa dharura.
Mkurugenzi mkuu wa idara ya afya Dr. Patrick Amoth, amesema pana haja ya kuzuia ugonjwa huo mapema ili kukabili kuenea kwake, akitolea mfano wa virusi vya Korona.
Haya yanajiri baada ya ugonjwa huo kuripotiwa nchini mwezi jana ingawa mgonjwa huyo aliyekuwa safarini kuelekea Rwanda kutoka Uganda, ameripotiwa kupona.
Imetayrishwa na Antony Nyongesa