MASOMO VYUONI YASAMBARATISHWA NA MGOMO
Shughuli za masomo katika vyuo vikuu vya umma kote nchini zimesambaratika kwa mara nyingine tena kufuatia mgomo wa wahadhiri wanaolalamikia madai ya kupuuzwa na serikali.
Kupitia kwa muungano wao wa UASU, wahadhiri wameitaka serikali kutekeleza mkataba wa maelewano waliotia Saini mwezi mmoja uliopita na wizara ya leba.
Mkataba huo ulitiwa Saini katika juhudi za serikali kumaliza mgomo uliokuwa umelemaza masomo vyuoni kwa takribani wiki mbili, na hadi sasa wahadhiri wanashikilia kuwa makubaliano hayo.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 







































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































