MAKATAA YA OMBUDSMAN KWA SAKAJA

Afisi ya utawala wa haki ya kisheria maarufu kama Ombudsman, imetoa makataa ya siku saba kwa gavana wa Nairobi Johnson Sakaja kufafanua upangaji upya wa jiji la Nairobi baada ya Sakaja kukosa kumjibu mkazi aliyetaka ufafanuzi huo.
Kwa mujibu wa afisi hiyo, mkazi mmoja mnamo mwezi Februari, alimtaka Sakaja kueleza ni lini uamuzi wa kujenga majumba yenye hadi ghorofa 75 katika baadhi ya sehemu za jiji uliafikiwa.
Mkazi huyo aidha, ametaka kufahamu iwapo miongozo hiyo mipya iliidhinishwa na Bunge la kaunti ya Nairobi.
Imetayarishwa na: Antony Nyongesa