KENNEDY ALIUAWA NA POLISI RONGAI WAKATI WA MAANDAMANO

Mwanapathologia wa serikali Peter Ndengwa aliyeufanyia mwili wa Kennedy Onyango upasuaji amebaini kuwa kennedy aliaga dunia kutokana na jeraha mbaya la risasi.
Mtoto huyo mwenye umri wa miaka 12 ambaye alipoteza Maisha yake wakati wa maandamano siku ya alhamisi eneo la Rongai kaunti ya Kajiado alipigwa risasi wakati wa maandamano hayo alipokuwa akielekea kwa rafikiye kuomba kitabu.
Imetayarishwa na Janice Marete