SUSWA: IPOA YAAHIDI HAKI KWA WAATHIRIWA
Katika juhudi za kurejesha utulivu na mshikamano katika eneo la Suswa kaunti ya Narok, mamlaka ya kutathmini mienendo ya maafisa wa polisi IPOA imesema inafanya uchunguzi wa kina kwenye mauaji ya watu wawili eneo hilo mwishoni mwa juma lililopita.
Kwa mujibu wa mamlaka hiyo, haki itapatikana kwa waathiriwa baada ya uchunguzi kukamilika kwenye machafuko hayo yaliyosababisha afisa wa polisi kukatwa mkono.
Maafisa wa IPOA wamezungumza baada ya kuwatembelea waathiriwa katika hospitali ya rufaa ya Narok.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 



































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































