#Local News

WAZIRI KINDIKI NDIYE NAIBU MPYA WA RAISNDIYEWAZIRI KINDIKI NDIYE NAIBU MPYA WA RAIS

Rais William Ruto amemteua waziri wa maswala ya ndani ya nchi Prof. Kithure Kindiki kuchukua nafasi ya aliyekuwa Naibu Rais Rigathi Gachagua, ambaye alitimuliwa na Bunge.

Prof. Kindiki, ambaye kwa sasa anahudumu kama Katibu wa Baraza la Mawaziri wa Mambo ya Ndani na Utawala wa Kitaifa, atahitaji idhini kutoka kwa Bunge la Kitaifa kabla ya kuchukua rasmi nafasi ya Naibu Rais. Bunge lazima lipigie kura uteuzi ndani ya siku 60 baada ya kupokea jina lake.

Baada ya kuidhinishwa, mteule atateuliwa rasmi na Rais kuwa naibu wake.

Ingawa Katiba haijaweka bayana muda wa uteuzi huu, unatarajiwa kutokea mara baada ya kuidhinishwa na Bunge.

Imetayarishwa na Janice Marete

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *