#Local News

JUHUDI ZA KUBORESHA AFYA

Kama njia moja ya kulainisha utoaji huduma za afya kwa wakenya, kamati ya afya katika bunge la kitaifa imependekeza kubuniwa kwa tume ya huduma za afya itakayosimamia sekta hiyo.

Mapendekezo hayo yamejiri wakati wa kikao cha kamati hiyo inayoongozwa na mwenyekiti wake mbunge wa Endebess Robert Pukose na jopokazi la watu 20 linaloendelea kupokea maoni kuhusiana na jinsi ya kuboresha sekta ya afya nchini.

Jopokazi hilo lililoteuliwa na Rais William Ruto Julai mwaka jana, litatoa ripoti yake mwezi ujao.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

JUHUDI ZA KUBORESHA AFYA

AFUENI KWA JAJI KULLOW

JUHUDI ZA KUBORESHA AFYA

WANAFUNZI WAVAMIA HELB KUDAI MIKOPO

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *