REKODI YA TIGIST YAIDHINISHWA

Rekodi Ya Dunia Ya Mbio Za Marathon Ya mwanariadha Tigist Assefa Ya Saa 2 Dakika 11 Na Sekunde 53 Iliyowekwa Katika Berlin Marathon Mwaka Jana Imeidhinishwa Rasmi Na shirika la Riadha la Dunia.
Mwathiopia Huyo Alivunja Alama Ya Awali Kwa Zaidi Ya Dakika Mbili Mnamo Septemba 24, Na Kufuta Rekodi Ya Dunia Ya Saa 2:14:04 Iliyowekwa Na Brigid Kosgei Wa Kenya Mjini Chicago Oktoba13, 2019.
Amesema kwa anatumai Kwamba Uchezaji Wangu Utakuwa Motisha Kwa Wanariadha Wa Kike Nchini Ethiopia Na Kwamba Rekodi Ya Dunia Mwaka Mmoja Kabla Ya Michezo Ya Olimpiki Itaipa Nchi Yake Nguvu Kule Paris,
Muda Wa Ushindi Wa Assefa Ulikuwa Rekodi Ya 13 Ya Dunia Kuwekwa Mjini Berlin.