#Local News

KAUNTI YA BARINGO CHINI YA UCHUNGUZI WA SENETI DHIDI YA AKAUNTI 304 ZA BENKI

Bunge limeiagiza Serikali ya Kaunti ya Baringo kutoa stakabadhi zinazoelezea makubaliano kati ya kaunti hiyo, Mdhibiti wa Bajeti na Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu kuhusu kufunguliwa kwa akaunti 304 za benki kinyume cha sheria.

Maseneta walitoa agizo hilo jana Jumatatu Gavana wa Baringo Benjamin Cheboi alipofika mbele ya Kamati ya Seneti kuhusu Ugatuzi na Mahusiano ya Kiserikali.

Gavana huyo amepewa makataa ya siku mbili kutekeleza agizo hilo kama ilivyoainishwa katika Sheria ya Usimamizi wa Fedha za Umma (PFM).

Seneta wa Kisii Richard Onyonka alihoji jinsi kaunti hiyo ilifungua akaunti nyingi za kutumia pesa za DANIDA, akidokeza kuwa kuna uwezekano kwamba pesa zingine zilitolewa kinyume cha sheria.

Imetayarishwa na Janice Marete

KAUNTI YA BARINGO CHINI YA UCHUNGUZI WA SENETI DHIDI YA AKAUNTI 304 ZA BENKI

TIMU ZAPATA UFADHILI

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *