#Local News

MZOZO WA UONGOZI WAENDELEA CHUONI

Baraza la chuo kikuu cha Nairobi kupitia mwenyekiti wake Amukoa Anangwe, limeshikilia kwamba mkuu wa chuo hicho Profesa Stephen Kiama yuko nje kwa likizo ya lazima.

Kwa mujibu wa Anangwe, baraza hilo linatilia manani kuenea kwa unyanyasaji, udhalilishaji wa wafanyakazi na matumizi mabaya ya raslimali za chuo hicho.

Aidha, amesema mahakama ya uajiri na leba ilitoa agizo la kusitisha mageuzi ambayo yamekuwa yakiendelea katika chuo hicho, huku Profesa Ayub Njoroge Gitau akiteuliwa kuwa kaimu mkuu.

Imetayarishwa na: Antony Nyongesa

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *