MAN CITY YAILAZA WOLVES 2-1 DAKIKA ZA LALA SALAMA NA KUWA KILELENI
Beki wa Manchester City John Stones alifunga kwa kichwa bao la ushindi wa dakika za mwisho katika ushindi wa 2-1 dhidi ya Wolverhampton Wanderers jana Jumapili na kuwaweka kileleni mwa Ligi ya Premia na kuweka rekodi ya klabu ya mechi 31 za ligi bila kufungwa.
Mabingwa City walitawala mpira kuanzia mwanzo hadi mwisho lakini walishtuka dakika ya saba wakati krosi nzuri kutoka kwa Nelson Semedo ilipokutana na mshambuliaji wa Wolves Jorgen Strand Larsen.
Semedo alipoteza nafasi adhimu ya kuwaweka Wolves mbele zaidi kwa bao moja-kwa-moja ambalo Ederson aliokoa, kabla ya beki wa City, Josko Gvardiol kuchukua mpira angani na kufumua shuti zuri lililopita kwa Jose Sa na kusawazisha bao lililostahili dakika ya 33.
Bao la Stone la dakika za lala salama lilienda kwa ukaguzi wa Video Assistant Referee (VAR), na likaruhusiwa, jambo lililomfurahisha meneja wao Pep Guardiola na mashabiki waliosafiri.
City walisonga kileleni kwa tofauti ya mabao wakiwa na pointi 20, mbili juu ya Liverpool Wolves wako mkiani kwa pointi moja na hawajapata ushindi wowote msimu huu.
Imetayarishwa na Janice Marete
English 





























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































