MCAS TAITA WASUTWA BAADA YA KUMBANDUA SPIKA
Wiki moja baada ya spika wa bunge la kaunti ya Taita Taveta Wisdom Kazungu kubanduliwa baada ya wawakilishi wadi kukosa imani katika utendakazi wake, baadhi ya wakazi, wanaharakati na viongozi kwenye kaunti hiyo wamekosoa hatua hiyo.
Wamedai kwamba wawakilishi hao walikuwa na njama ya kutetea maslahi yao na wala si ya wananchi.
Wakizungumza mjini Voi, wamesema kwamba misingi iliyotumiwa kumbandua spika huyo haina uzito wowote.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































