#Local News

UNYANYAPAA, UBAGUZI WAIPONZA SHULE

Jopo la majaji watano linaloshughulikia ubaguzi dhidi ya waathiriwa wa ugonjwa wa UKIMWI limeiagiza shule ya msingi ya Najah iliyoko katika kaunti ya Garissa kumfidia mwanamke mmoja shilingi elfu 650 kutokana na unyanyapaa na ubaguzi aliofanyiwa mwanawe aliye na virusi vya UKIWMI.

Jopo hilo linaloongozwa na Caroline Mboku, limetoa uamuzi huo baada ya kubainika kwamba uongozi wa shule hiyo ulimpa mwanamke huyo shilingi elfu 10 ili kumwondoa mwanawe shuleni humo baada ya kugundua kuwa mwanafunzi huyo alikuwa na virusi vya UKIMWI.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

UNYANYAPAA, UBAGUZI WAIPONZA SHULE

WAFUNGWA KWENYE KESI YA THUO KUHUKUMIWA JUNI

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *