KISIA AINGIA IMPALA
Kocha msaidizi wa timu ya taifa ya Kenya raga ya wachezaji saba kwa wanaume, Louis Kisia anatarajiwa kuteuliwa kocha mkuu mpya wa Impala Club.
Kisia alijiuzulu kama kocha mkuu wa Strathmore Leos mwezi Machi mwaka huu na tangu wakati huo amekuwa na kazi ngumu na timu ya taifa lakini sasa atarejea katika raga ya klabu na Impala yenye makao yake Ngong-road.
Kisia anasema amepata ofa kadhaa za kurejea katika ufundishaji wa raga ya vilabu lakini akachagua kuchukua kazi ya Impala kwa sababu ya mradi ambao timu hiyo inaufanyia kazi ili kurejea kwenye raga ya ligi kuu.
Kwasasa Impala wako kwenye ligi ya daraja la pili na Kisia atakuwa na kibarua sawa na alichokifanya akiwa Strathmore Leos – kujaribu kurudisha timu hiyo ligi kuu.
Washindi hao mara 10 wa ligi kuu walishushwa daraja mwishoni mwa msimu wa 2021/2022 na wanawania kujinyanyua tena wakiongozwa na Kisia.
Imetayarishwa na Nelson Andati
English 











































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































