#Sports #Volleyball

MALKIA STRIKERS WASEMA WAKO TAYARI

Nahodha wa Malkia Strikers, Trizah Atuka amesema timu iko tayari kwa majukumu ya Kombe la FIVB Challenger na Michezo ya Olimpiki.

Atuka mwenye umri wa miaka 32 ana uhakika mabingwa hao mara kumi wa Afrika watatangaza uwezo wao katika majukumu hayo mawili licha ya kuonekana kuwa wanyonge.

Atuka amewapongeza wadhamini ambao wamejitokeza ili kuongeza maandalizi yao kabla ya majukumu hayo mawili.

Kocha mkuu Japheth Munala anasema licha ya kupangwa dhidi ya miamba duniani, hawatakwenda kwenye michuano hiyo kama washiriki bali washindani.

Malkia Strikers wamepangiwa kuondoka kwa Kombe la Challenger litakaloanza Julai 4 nchini Ufilipino kabla ya kupiga kambi Miramas, Ufaransa kabla ya Michezo ya Olimpiki ya Paris.

Imetayarishwa na Nelson Andati.

MALKIA STRIKERS WASEMA WAKO TAYARI

RUTO ATII SHINIKIZO ZA MSWADA

MALKIA STRIKERS WASEMA WAKO TAYARI

KENYA MORAN WATIA FORA

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *