MATOKEO NI YA WALIMU, SI WANAFUNZI- WAKAZI BUSIA
Wakazi wa Bumala kaunti ya Busia wamefanya maandamano kulalamikia matokeo duni yaliyorekodiwa na watahiniwa wa mtihani wa KCSE katika shule ya Bumala B, wakiulaumu usimamizi wa shule hiyo kwa matokeo hayo.
Wakizungumza baada ya maandamano, wakazi hao wameshinikiza mageuzi katika usimamizi wa shule hiyo.
Kwenye mtihani huo, shule hiyo ilipata alama ya wastani ya 3.23, watahiniwa wakiwa 122, watahiniwa 3 pekee wakipata alama ya kuwawezesha kujiunga na chuo kikuu.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































