AMOLLO ATISHIA MSUMARI WA MWISHO KWA GACHGUA
Mbunge wa Rarieda Otiende Amollo ametishia kuwasilisha mswada bungeni kwa lengo la kumpiga marufuku aliyekuwa naibu Rais Rigathi Gachagua dhidi ya kuwania afisi yoyote ya umma.
Otiende ambaye anamtuhumu Gachagua kwa madai ya kueneza siasa za migawanyiko, amesema kuwa Gachagua hajapata funzo lolote kutokana na kutimuliwa kwake kutoka afisini mwaka jana.
Ametishia kuwa iwapo Gachagua hatasitisha mwenendo unaodaiwa, basi bunge litamchukulia hatua chini ya sehemu ya 3 ya kipengee cha 75 cha katiba ya Kenya kinachomzuia yeyote aliyetimuliwa kutoka afisini kuwania wadhifa wowote wa umma.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































