GACHAGUA AMEKWAMISHA MAENDELEO, WAKAZI BUNGOMA

Wakati uo huo, vikao vya kukusanya maoni kuhusu kubanduliwa kutoka afisini kwa naibu Rais Rigathi Gachagua katika eneo bunge la Webuye Magharibi kaunti ya Bungoma vimeandaliwa katika eneo la Matisi ambako wakazi wametoa maoni kinzani kuhusiana na mchakato huo.
Wakazi ambao wameunga mkono kutimuliwa kwa Gachagua wamemshutumu kwa madai ya kwamba naibu huyo wa rais hana heshima kwa Rais William Ruto, na kwamba amechangia kukwama kwa miradi ya serikali.
Hata hivyo, baadhi wamepinga wakisema huenda mjadala huo ukasbabisha kuanza kwa siasa za mapema na hivyo na hivyo kuathiri maendeleo ya taifa.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa