WANAFUNZI WALALAMIKIA KATEGORIA TATA

Hazina ya kufadhili elimu ya juu imepokea malalamishi kutoka kwa wanafunzi zaidi ya 10,000 wanaotarajia kujiunga na vyuo vikuu, wakisema wamewekwa katika kategoria ambazo haziwiani na mapato ya familia zao.
Mkurugenzi mkuu wa hazina hiyo George Munari amesema kuwa zoezi la kukagua malalamishi hayo litachukua muda wa wiki tatu.
Aidha, ametoa wito kwa usimamizi wa vyuo vikuu vya umma kuendelea kuwasajili wanafunzi wanaposubiria ufadhili kutolewa.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa