VERONICA MUENI NDUVA ATEULIWA KUWA KATIBU MKUU WA EAC
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) Veronica Mueni Nduva, amesema kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi unaochochea uvumbuzi, ujasirimali na utoaji wa nafasi za ajira pamoja na amani na usalama zitapewa kipaumbele
Nduva ameyasema hayo baada ya kuapishwa katika Mkutano wa 23 wa Wakuu wa EAC uliofanyika Ijumaa iliyopita.
Nduva vile vile amesema muhula wake utajikita zaidi katika kuboresha ushirikiano wa kina na maendeleo ya watu wa Afrika Mashariki.
Ameongeza kuwa maendeleo ya kisasa ya kijamii yatapewa kipaumbele katika uongozi wake, huku nafasi kubwa ikitolewa katika kuwawezesha wanawake na vijana, ambao ni msingi wa jamii katika kanda hii.
Nduva anachukua nafasi ya Peter Mathuki ambae ametwikwa majukumu mengine na serikali ya kitaifa ya Kenya.
Imetayarishwa na Maureen Amwayi.
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































