WAZIRI MBADI KUSOMA MAKADIRIO YA BAJETI

Wakenya wameelekeza macho yao kwa bunge la kitaifa hii leo wakati ambapo waziri wa fedha John Mbadi atasoma makadirio ya bajeti ya shilingi trilioni 4.2 ya mwaka wa kifedha wa 2025-26, hii ikiwa ndiyo bajeti yake ya kwanza tangu ateuliwe kuwa waziri.
Makadirio hayo ni kiasi cha juu zaidi kuwahi kusomwa nchini, shilingi trilioni 1.79 zikitengewa matumizi ya kila siku, shilingi bilioni 707 ziktengewa maendeleo, nalo slaio la shilingi trilioni 1.34 zikitumika kuliapa madeni ya taifa.
Huyu hapa waziri Mbadi akizungumza na wafanyabiashara hapo jana.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa