RAIS RUTO KUZINDUA AZMA YA ODINGA WIKI IJAYO

Azma ya kinara wa ODM Raila Odinga kuwania uwenyekiti wa tume ya umoja wa Afrika AUC inatarajiwa kushika kasi, baada ya mkuu wa mawaziri Musalia Muadavadi kutangaza kwamba Rais William Ruto atazindua rasmi azma ya Odinga wiki ijayo.
Akizungumza na wanahabari muda mfupi uliopita, Mudavadi amemsifia Raila, akisema kiongozi huyo amekuwa akiwakilisha matamanio ya wakenya na kuwataka kumuunga mkono.
Aidha, Mudavadi amempongeza Rais Ruto na serikali yake kwa kuunga mkono uwaniaji wa Odinga.
Kwa upande wake, Odinga ameridhia uamuzi wa serikali kuunga mkono azma yake, akisema kwamba yuko tayari kulitumikia bara hili.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa