SIKU 2 KUU ZA GAVANA GUYO ZAANZA
Siku 2 za kuamua hatma ya gavana wa Isiolo Abdi Guyo zinaanza hii leo wakati gavana huyo atawasili katika bunge la seneti kujitetea dhidi ya madai ya ufisadi na utumiaji mbaya wa afisi yaliyosababisha wawakilishi wadi katika bunge la kaunti hiyo kumbandua.
Bunge la seneti wiki jana liliafikia kuandaa kikao cha maseneta wote badala ya kamati kusikiliza kesi hiyo ambayo imeratibiwa kuanza kusikilizwa muda wowote kuanzia sasa.
Uamuzi wa wawakilishi wadi hao kumbandua gavana Guyo utadumishwa tu iwapo maseneta wasipoungua 24 watapiga kura kuunga mkono hoja ya kumbandua.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 












































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































