#Athletics #Sports

TUWEI ANA MIPANGO YA KUMRITHI SEBASTIAN COE

Rais wa shirikisho la Riadha nchini (AK) Lt. Jenerali (Mst) Jackson Tuwei ameweka nia yake moyoni mwake kuhusu uwezekano wa kumrithi Lord Sebastian Coe kama rais wa shirikisho la riadha ulimwenguni, iwapo Coe atachaguliwa rais wa Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki (IOC).

Tuwei, ambaye pia anahudumu kama Makamu wa Rais wa shirikisho hilo duniani, ameongoza AK katika kipindi kilichoadhimishwa na matukio ya sifa kuu kimataifa, akikuza wasifu wake kama rais anayetarajiwa wa shirikisho hilo.

Mashindano ya Dunia ya Vijana walio chini ya umri wa miaka 18 mwaka wa 2017, Mashindano ya Dunia ya Vijana walio chini ya umri wa miaka 20 mwaka wa 2021, Kipchoge Keino Classic na World Cross Country Tour (Sirikwa) yote yamefanyika nchini Kenya katika enzi ya Tuwei.

Kumbuka kwamba Waziri wa Michezo Kipchumba Murkomen, ametangaza kuwa AK itafanya uchaguzi mwaka ujao, na kuashiria mwisho wa uongozi wa Tuwei.

Imetayarishwa na Nelson Andati

TUWEI ANA MIPANGO YA KUMRITHI SEBASTIAN COE

LEE AWAITA WACHEZAJI WAWILI KIKOSINI

TUWEI ANA MIPANGO YA KUMRITHI SEBASTIAN COE

MAKALA YA CHEMUSUSU YAZINDULIWA RASMI

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *