#Local News

WAKAAZI MUMIAS WASHUTUMU POLISI

Wakazi wa Mumias Mashariki kaunti ya Kakamega wamewashutumu maafisa ya polisi katika kituo cha polisi cha Shianda kwa madai kwamba maafisa hao wameshindwa kukabili uhalifu eneo hilo.

Wakiongozwa na David Wamatsi, wakazi wamewalaumu polisi kwa kukosa kumchukulia hatua mshukiwa wa mauaji ya mkazi mmoja kwa kumgonga na pikipiki yapata miezi miwili iliyopita.

Wakazi hao sasa wameahidi kushinikiza maafisa wa polisi kwenye kituo hicho wapewe uhamisho.

Hata hivyo, mkuu wa polisi wa Shianda Doris Chemos amekana madai ya kushirikiana na wahalifu, akisema uchunguzi kwenye mauaji hayo unaendelea.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

WAKAAZI MUMIAS WASHUTUMU POLISI

HATUNA UBAYA NA WENZETU, MUNYA

WAKAAZI MUMIAS WASHUTUMU POLISI

MASENGELI ASHIKA USUKANI

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *