SUDI AONDOLEWA KESI YA KUGHUSHI
Mbunge wa Kapsaret Oscar Sudi amepata afueni baada ya mahakama hiyo ya ufisadi kumwondolea mashtaka ya kughushi stakabadhi za masomo.
Hakimu Felix Kombo amesema upande wa mashtaka umeshindwa kuwasilisha Ushahidi wa kuipa uzito kesi hiyo, akiongeza kuwa wameshindwa kuthibitisha madai ya kughushi dhidi ya Sudi.Aidha, ameulamu upande wa mashtaka kutokana na jinsi ulivyopata sehemu ya Ushahidi, akisema ni ya kutiliwa shaka
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































