#Sports

LEVY APIGIA UPATO TOTTENHAM KUCHUKUA LIGI MSIMU MPYA

Mwenyekiti wa Tottenham Daniel Levy alisema hajutii kumwajiri Ange Postecoglou huku akitetea uamuzi wa kumfukuza kocha huyo raia wa Australia.

Postecoglou aliiongoza Spurs kutwaa taji lao la kwanza kwa miaka 17 kwa kushinda Ligi ya Europa mwezi uliopita.

Hata hivyo, hiyo haikutosha kuokoa kibarua chake baada ya kumaliza katika nafasi ya 17 kwenye Premier League. Uamuzi wa kumfukuza kocha huyo wa zamani wa Celtic na kumteua Thomas Frank umekabiliwa na upinzani kutoka kwa mashabiki wengi wa Tottenham.

Lakini Levy alielezea matarajio yake kwa Spurs kuwa washindi wa Ligi Kuu na Ligi ya Mabingwa siku moja.

Tottenham haijashinda ligi kuu ya Uingereza tangu 1961 na haijawahi kushinda Ligi ya Mabingwa.

“Tumeshinda kombe la Uropa, lakini haitoshi,” Levy aliongeza.

“Ni jambo ambalo hatujafanya ambalo ni muhimu zaidi. Tunahitaji kushinda ligi. Tunataka kushinda Ligi Kuu. Tunataka kushinda Ligi ya Mabingwa. Tunataka kushinda.”

Levy ameshikilia wadhifa wake Tottenham kwa zaidi ya miaka 25 huku Frank akiwa meneja wa 13 wa kudumu wakati huo.

“Kila unapokuwa na kocha mpya, huwa ni mwanzo mpya. (Wapo) huwa na mawazo tofauti lakini tunataka kuendeleza mafanikio ya kutwaa kombe msimu uliopita,” alisema.

“Mojawapo ya mambo ambayo yalinivutia sana na Thomas ni kwamba ana akili nyingi sana, ni mzungumzaji mzuri, binadamu bora pamoja na vipengele vyote vya kiufundi ambavyo ni muhimu kwa wazi.”

Imetayrishwa na Nelson Andati

LEVY APIGIA UPATO TOTTENHAM KUCHUKUA LIGI MSIMU MPYA

OJWANG AREJEA KIKOSINI

LEVY APIGIA UPATO TOTTENHAM KUCHUKUA LIGI MSIMU MPYA

INZAGHI AWAPUZULIA MBALI WAKOSOAJI

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *