USHURU KWA SODO? JAMANI!!!!

Mbunge wa Embakasi mashariki Babu Owino ameendea kukashifu serikali ya rais William Ruto Pamoja na mapendekezo ya mswada wa fedha.
Akihojiwa katika kituo kimoja cha radio humu nchini babu amesikitikia hatua ya serikali kutaka kutoza kodi vitambaa vya hedhi yaani sodo bila kujali mathara yake kwa wasichana na kina mama huku kukiwa na tetesi kwamba zaidi ya asilimia 60 ya wasichana hawawezi kumudu gharama ya kununuja sodo.
Babu aidha amewahimiza wakenya kutumia mitandao ya kijamii kuwashinikiza wabunge wao kuangusha mswada wa fedha.
Imetayarishwa na Janice Marete