KESI DHIDI YA GACHAGUA YAONDOLEWA MAHAKAMANI

Mahakama kuu imeondoa kesi iliyowasilishwa dhidi ya Naibu Rais Rigathi Gachagua kuhusiana na matamshi ya Gachagua dhidi ya mkurugenzi wa idara ya ujasusi wa kitaifa yaani NIS Noordin haji.
Jaji John Chigiti amesema kesi hiyo iliyokuwa imeratibiwa kutajwa leo na kutoa mwelekeo zaidi, imeondolewa kupitia notisi ya mwanaharakati Fredrick Bikeri aliyekuwa ameiwasilisha kesi hiyo.
Kwenye kesi hiyo, Bikeri alihoji kwamba matamshi ya Gachagua ya kumlaumu Haji kuhusiana na vurugu zilizoshuhudiwa wakati wa maandamano hayafai kutolewa na afisa wa serikali.
Imetyarishwa na Antony Nyongesa