#Sports #Volleyball

KVF YATAFUTA KOCHA WA MALKIA STRIKERS

Shirikisho la Mpira wa Voliboli la Kenya (KVF) linatafuta kocha mkuu mpya wa timu ya taifa ya wanawake ya voliboli, Malkia Strikers, kuelekea Mashindano ya Dunia ya Wanawake ya FIVB 2025 yatakayofanyika kuanzia Agosti 22 hadi Septemba 7, mwaka huu nchini Thailand.

KVF ilitangaza kuwa inakaribisha maombi kutoka kwa wale wanaopenda kushika nafasi ya kocha mkuu, makocha wawili wa wasaidizi, na mzoezaji wa mwili, ambapo usaili umepangwa kufanyika tarehe 15 Februari.

Kocha mzoefu Japheth Munala, ambaye pia ni kocha mkuu wa KCB, amekuwa akiongoza Malkia Strikers tangu Oktoba 2023 na aliipeleka timu hiyo katika Michezo ya Olimpiki ya Paris mwaka jana.

Kulingana na Katibu Mkuu wa KVF, Ismail Chege, shirikisho linatafuta kumtangaza kocha mpya wa benchi la kiufundi la Malkia Strikers kwa mkataba wa kudumu badala ya mkataba wa muda.

Janet Wanja, aliyekuwa mcheza mpira wa voliboli na ambaye alifariki kutokana na saratani ya kibofu cha mkojo mwezi jana, alikuwa pia sehemu ya benchi la kiufundi kama mzoezaji wa timu wakati wa Olimpiki za Paris.

Imetayarishwa na Janice Marete

KVF YATAFUTA KOCHA WA MALKIA STRIKERS

KENYA POLICE YASHINDA MARA SUGAR NA KUREJEA

KVF YATAFUTA KOCHA WA MALKIA STRIKERS

MANCHESTER UNITED YACHARAZA FULHAM 1-0

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *