OMBACHI ASUTA SHIRIKA LA RAGA

Nyota wa zamani wa timu ya taifa ya wachezaji saba, Dennis Ombachi ametoa wito kwa Muungano wa Raga nchini Kenya kutatua masuala ya kandarasi na wachezaji wa timu ya Sevens kabla ya kurejea kwao katika Msururu wa Raga wa Dunia wa Sevens.
Wachezaji wa Shujaa wamegoma kurejea mazoezini baada ya Safari Sevens kutokana na masuala ya kimkataba, na Ombachi anatoa wito kwa shirikisho hilo kushughulikia mkwamo huo haraka iwezekanavyo.
Ombachi pia alisisitiza juu ya umuhimu wa wachezaji kurejea mazoezini kujiandaa na mechi za Dubai na Cape Town, zilizopangwa kumalizika mwezi huu na mwezi ujao, akisema wanahitaji kasi ya hivi karibuni kuendelea, ili timu ipate matokeo mazuri.
Kulingana na Ombachi, matokeo mazuri yatakuja katika siku zijazo ikiwa timu itaungwa mkono vyema na wadau wote wa raga.
Imetayarishwa na Nelson Andati