GAVANA MWANGAZA AZIMIWA, TENA
Gavana wa Meru Kawira Mwangaza ametimuliwa afisini, kwa mara ya tatu katika muda wa miaka 2 baada ya wawakilishi wadi kupiga kura ya kumtimua kutokana na tuhuma za ukiukaji wa katiba, utovu wa nidhamu na matumizi mabaya ya afisi.
Hoja ya kumbandua mamlakani aliwasilishwa katika bunge hilo na naibu kiongozi wa walio wengi Zipporah Kinya, na kuungwa mkono na wawakilishi wadi 49 dhidi ya 17 waliopinga.
Gavana huyo atajua mwisho wake wakati hoja hiyo itawasilishwa katika bunge la seneti kuona iwapo uamuzi huo utabatilishwa au kudumishwa.
Imetayrishwa na Antony Nyongesa
English 































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































