UN MBIONI KUREJESHA UTULIVU DRC
Baraza la usalama la umoja wa mataifa limeandaa kikao cha pili kujadili hali tete iliyoko mashariki mwa taifa la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo DRC.
Mkutano huo umeitishwa na viongozi wa DRC kutokana na mapigano ya kundi la waasi la M 23 ambalo limeuteka mji wa Goma na uwanja wa ndege.
Waziri wa masuala ya kigeni wa DRC Therese Kayikwamba amekosoa agizo la baraza hilo kutaka vikosi vya kigeni vya usalama kuondoka nchini humo.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 











































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































