MAHAKAMA YAPINGA OMBI LA MAGAVANA KUHUSU MALIPO YA UZEENI
Magavana wamepata pigo baada ya mahakama kuu kuamuru kwamba magavana na manaibu wao hawana haki ya kupokea marupurupu ya uzeeni katika mpango sawa na ule wa maafisa wakuu katika serikali ya kitaifa.
Uamuzi huo umetolewa kufuatia kesi iliyowasilishwa na baraza la magavana dhidi ya tume ya kuratibu mishahara ya wafanyakazi wa umma SRC inayosema serikali haina uwezo wa kuwaorodhesha magavana na manaibu wao kwenye mpango huo.
Aidha, SRC inashikilia kwamba endapo ombi lao litatekelezwa, hatua hiyo itaathiri maafisa wakuu katika serikali za kaunti na ile ya kitaifa.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 







































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































