SERIKALI KUONDOA MADENI YA WAKULIMA WA KAHAWA

Waziri wa kilimo Mithika Linturi, ametangaza kwamba serikali inapanga kuondoa madeni ya shilingi bilioni 6 wanaodaiwa wakulima wa kahawa katika kikao kijacho cha baraza la mawaziri.
Akizungumza alipofika mbele ya seneti, Linturi aidha amejivunia hatua ambazo serikali imepiga katika kuimarisha uzalishaji wa mazao mbali mbali ikiwemo majani chai.
Kuhusu suala la mbolea ya kahawa kukosekana katika maghala ya bodi ya nafaka nchini, amekiri tatizo hilo na kusema serikali itahakikisha wakulima wanapata mbolea wanayohitaji kwa wakati unaofaa.
Imetayarishwa na: Antony Nyongesa
English 




























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































