SEKTA YA MIFUGO KUNUFAIKA KUPITIA MPANGO WA DRIVE

Sekta ya mifugo nchini imepata afueni baada ya Mpango wa DRIVE kutenga shilingi milioni 519 ili kupunguza hatari za ufugaji na kuongeza ushirikishaji wa jamii katika kuongeza thamani ya bidhaa za mifugo.
Mpango huu unaoongozwa na Shirika la Maendeleo la Kenya (KDC) kwa usaidizi wa Benki ya Dunia, umezinduliwa jijini Nairobi katika mkutano wa wadau na unalenga kuimarisha biashara ya ufugaji katika kaunti 20 zikiwemo Marsabit, Samburu, Narok na Kajiado.
Fedha hizo zitasaidia kuinua viwango vyote vya thamani ya mifugo kuanzia lishe, uchakataji wa nyama na ngozi, hadi biashara kwa kuzingatia maendeleo yanayoongozwa na jamii na yasiyoathiri tabianchi. Mpango huu unaleta matumaini mapya kwa maeneo kame na yaliyotengwa ambayo sasa yanaibuka kama vituo vya uwekezaji.
Imetayarishwa na Maureen Amwayi