FAMILIA YA NDUGU WA KITENGELA YAZUNGUMZA

Hatimaye familia ya ndugu wawili wa Kitengela waliokuwa wametoweka kwa mwezi mzima sasa imezungumza kwa mara ya kwanza tangu wawili hao wapatikane wiki jana.
Kulingana na Abdirazak Longton ambaye ni nduguye Jamil na Aslam Longton, wawili hao walinyimwa chakula na kuteswa, mbali na kunyimwa haki nyingine za kikatiba walipokuwa wakezuiliwa na wanaoaminika kuwa polisi.
Aidha, amesema ndugu zake walionywa dhidi ya kuzungumzia masaibu yao.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa