MAAFISA WATANO KORORKORONI KWA MAUAJI YA MTOTO WA MIAKA 19 BARINGO

Maafisa watano wa idara ya misitu wanaendelea kuzuiliwa baada ya kukamatwa jana jumanne eneo la maji mazuri kaunti ya baringo kwa madai ya kuhusika katika kifo cha Stephen Mwangi kijana mwenye umri wa miaka 19.
Inadaiwa kuwa Mwangi alikuwa amekwenda katika kituo cha misitu cha maji mazuri , kupeleka ada ya elfu 2 alizokuwa ametozwa mamake baada ya kukamatwa akitema kuni katika msitu huo.
Babaye marehemu John ambuka amesema mwanawe aliwapata maafisa hao watano wakimdhulumu mama yake na katika harakati za kumwokoa akamvamia na kupigwa kinyama.
Mwangi aliumizwa sehemu za kichwa na bavu hali iliyosababisha kifo chake akitibiwa katika hospitali ya rufaa ya moi.
English 









































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































